Category Archives: News

Mjumbe wa kamati ya siasa ya Chama cha mapinduzi (ccm)wilayani Kyela.

Mjumbe wa kamati ya siasa ya Chama cha mapinduzi (ccm)wilayani Kyela,Joseph Mwaipopo(65)mkazi wa kijiji cha Fubu kata ya Ikama amefikishwa Mahakama ya wilaya ya Kyela jana akituhumiwa kumbaka mtoto wa dada yake Dorris Hassan(21).
Mwendesha mashitaka wa jeshi wa polisi wilayani Kyela, Nicholaus Tiba aliiambia mahakama hiyo kuwa mnamo julai 16 mwaka huu mnamo majira ya saa 4 asubuhi mtuhumiwa alimbaka mtoto wa dada yake walipo kuwa kwenye shamba la matikiti ambako walikuwa wana mwagilia maji katika shamba hilo.
Amesema mlalamikaji baada ya kufanyiwa kitendo hicho alitoa taarifa katika ofisi ya Serikari ya kijiji cha Fubu na baada ya hapo walitoa taarifa katika kituo kidogo cha Polisi Ipinda ambao nao walimpeleka Hospitali kwa uchunguzi zaidi.
Mwendesha mashitaka huyo alimweleza hakimu mkuu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Joseph Luamsanao, kuwa mtuhumiwa amefikishwa katika mahakama hiyo chini ya kifungu kidogo cha kwanza na cha pili B na kifungu cha 131 chini ya kifungu kidogo cha kwanza cha makosa ya jinai sura ya 16 ya kanuni ya adhabu iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Mtuhumiwa amekana shitaka lake na yupo nje kwa dhamana ya watu wawili na kila mmoja kumdhamini mtuhumiwa kwa Tsh milioni 2.