Monthly Archives: May 2013

Ajali ya gari yaharibu miundombinu ya maji Mbeya

Lori Mbeya
Ajali imetokea katikati ya Mji wa Mbeya eneo la Mabatini iliyohusisha gari aina ya FAW lenye Namba T 852 ASQ mali ya Kampuni ya Mohamed Enterprises ambalo limeharibu miundombinu ya Maji na kusababisha Hospitali ya wazazi ya Meta kukosa maji kwa muda usiojulikana.

Fundi mkuu wa Mamlaka ya maji mjini Mbeya Mhandisi Silyvester Ngwale amesema wanafanya kila linalowezekana ili kurejesha huduma ya maji wa wagonjwa wakiwemo wazazi katika Hospitali ya wazazi ya Meta.

Licha ya kwamba ajali hii haijasababisha madhara kwa binadamu, lakini imesababisha miundombinu ya maji kwa baadhi ya maeneo nyeti mjini Mbeya.

Pamoja na uharibifu wa maji, fundi Ngwale amesema watahakikisha wanatumia njia mbadala kuwepo kwa maji hospitali ya wazazi ya Meta.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda

Pinda1(1)

Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajia kuongoza mamia ya watu katika maziko ya watu watatu waliopoteza maisha kufuatia mlipuko ulitokea katika kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi ambao wanatarajiwa kuzikwa katika eneo la kanisa hilo leo.

Tayari mamia ya watu wameshawasili katika eneo la kanisa hilo kwa ajili ya kuanza misa takatifu ya mazishi ambayo itaambatana na zoezi la kuweka miili ya marehemu hao katika nyumba za milele.

Katika eneo ambalo maziko hayo yatafanyika punde ulinzi na usalama umeimarishwa katika kila pembe kwa lengo lakuhakikisha zoezi la maziko linaenda vizuri bila hofu miongoni mwa washiriki waliofika katika misa hiyo maalumu.

Viongozi wa dini waliotoka katika madhehebu mbali mbali pamoja na viongozi mbali mbali wanatarajia kushiriki katika misa hiyo ambapo tayari Waziri wa Mambo ya Ndani Dk Emanuel Nchimbi ameshawasili.

Sechelela Kongola, TBC Arusha.