Ajali ya gari yaharibu miundombinu ya maji Mbeya

Lori Mbeya
Ajali imetokea katikati ya Mji wa Mbeya eneo la Mabatini iliyohusisha gari aina ya FAW lenye Namba T 852 ASQ mali ya Kampuni ya Mohamed Enterprises ambalo limeharibu miundombinu ya Maji na kusababisha Hospitali ya wazazi ya Meta kukosa maji kwa muda usiojulikana.

Fundi mkuu wa Mamlaka ya maji mjini Mbeya Mhandisi Silyvester Ngwale amesema wanafanya kila linalowezekana ili kurejesha huduma ya maji wa wagonjwa wakiwemo wazazi katika Hospitali ya wazazi ya Meta.

Licha ya kwamba ajali hii haijasababisha madhara kwa binadamu, lakini imesababisha miundombinu ya maji kwa baadhi ya maeneo nyeti mjini Mbeya.

Pamoja na uharibifu wa maji, fundi Ngwale amesema watahakikisha wanatumia njia mbadala kuwepo kwa maji hospitali ya wazazi ya Meta.